Biden alivunja makubaliano yetu na Taliban: Pence





Aliyekuwa makamu wa rais wa zamani wa Marekani Mike Pence amejiunga na wale wanaokosoa jinsi Marekani ilivyoondoa majeshi yake Afghanistan, huku maoni yake yakichapishwa katika Jarida la Wall Street.
Akiita kilichotokea kuwa "udhalilishaji wa sera za kigeni tofauti na kitu chochote nchi yetu imevumilia tangu mgogoro wa mateka wa Iran", Bw. Pence alidai Rais Joe Biden alikuwa amevunja mpango wa makubaliano ambao utawala uliopita ulikuwa umekubaliana na Taliban.

Mkataba huo, Bwana Pence alisema, ulikuwa ni kuondoka wanajeshi wa Marekani hatua kwa hatua kutoka Afghanistan maadamu Taliban ilisitishe mashambulizi dhidi ya wafanyikazi wa Marekani, ikatae kuwa eneo salama kwa magaidi na kujadiliana na viongozi wa Afghanistan juu ya kuunda serikali mpya.

Bwana Pence alidai kwamba Rais Biden alivunja mpango huo kwa kutangaza kwamba vikosi vya Marekani vitasalia Afghanistan kwa miezi kadhaa zaidi, na kwamba hii ilichochea Taliban kuanza mashambulizi yao.

Lakini wengine tayari wameanza kukataa tabia iliyojitokeza ya utendaji matukio namna hii.

Msomi na mwandishi wa habari Thomas Joscelyn ameelezea kuwa Taliban walishindwa kutimiza masharti kadhaa vile vile, ingawa alikubali kwamba wapiganaji wengi walijizuia kuwashambulia Wamarekani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad