Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) alikutana kisiri na kiongozi wa Taliban huko Kabul Jumatatu, vyanzo vimeviambia vyombo vya habari vya Marekani Taliban kuwa CIA hawajathibitisha mkutano huo ulioripotiwa kati ya William Burns na Mullah Baradar.
Rais wa Marekani Joe Biden ameweka tarehe ya mwisho ya Agosti 31 kwa vikosi vya nchi yake kuondoka Afghanistan. Washirika - pamoja na Uingereza - wanataka muda huo kuongezwa .
Vikosi vya Marekani vimekuwa nchini Afghanistan tangu 2001, kufuatia mashambulio ya 9/11.Vyanzo vimeambia vituo vya habari vya Marekani , pamoja na New York Times, Washington Post, Associated Press na NPR juu ya mkutano wa CIA na Taliban.
Lakini hakuna maelezo ya kutosha kuhusu mkutano huo .
Ikiwa itathibitishwa, yatakuwa ni mawasiliano ya kiwango cha juu kati ya Marekani na Taliban tangu wanamgambo hao walipoichukua Kabul mnamo 15 Agosti, na kusababisha serikali ya Afghanistan inayoungwa mkono kimataifa kutoroka .
Karibu wanajeshi 5,800 wa Markani wanalinda uwanja wa ndege wa Kabul wakati maelfu ya raia wa kigeni na Waafghan wanajaribu kuondoka nchini.
Jarida la Washington Post linasema majadiliano hayo yanaweza kuwa yamehusisha tarehe ya mwisho ya jeshi la Marekani kumaliza opareseni yake ya kuwaondoa watu nchini humo.Pia Jumanne, Taliban walisema hakuna tena Waafghanistan watakaoruhusiwa kuondoka nchini, wala tarehe ya mwisho ya kujiondoa kwa Marekani haitabadilishwa ili waongeweze muda .
Mullah Baradar ni mmoja wa watu wanne ambao walianzisha kundi la Taliban mnamo 1994.Alikamatwa katika operesheni ya Marekani na Pakistani mnamo 2010 na alihudumia miaka minane gerezani.
Tangu 2019, amekuwa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Taliban huko Qatar.
Mnamo Februari 2020, alisaini makubaliano ya Doha juu ya kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani na Nato nchini Afghanistan .
Alikuwa pia kiongozi wa kwanza wa Taliban kuwasiliana moja kwa moja na rais wa Marekani, baada ya kufanya mazungumzo ya simu na Donald Trump mnamo 2020.Mullah Abdul Ghani Baradar ni nani?
Mullah Abdul Ghani Baradar ni mmoja ya watu wanne walioanzisha kundi la Taliban nchini Afghanistan 1994.
Alipanda na kuwa mtu muhimu wa kundi hilo baada ya Taliban kufurushwa nchini Afghinistan na Marekani 2001.
Alikamatwa kupitia uvamizi wa pamoja uliotekelezwa na Marekani wakishirikiana na Pakistan , kusini mwa mji wa Pakistan wa Karachi mnamo mwezi Februari 2010.
Hakusikika tena hadi mwaka 2012 wakati jina lake lilipoorodheshwa katika orodha ya wafungwa wa Taliban ambao serikali ya Afghan ilitaka kuwaachilia ili kuvutia mazungumzo ya amani.Pakistan baadaye ilimuachilia Baradar tarehe 21 Septemba lakini haijulikani alienda kuishi wapi.Wakati wa kukamatwa kwake alidaiwa kuwa naibu wa kiongozi wa kidini wa kundi hilo Mullah Mohammad Omar, na mmoja ya makomanda aliyemuamini sana.
Viongozi wakuu wa Afghanistan walikuwa na matumaini kwamba mtu kama yeye angeweza kulishawishi kundi la Taliban kufanya mazungumzo na serikali ya Kabul - mpango wa serikali uliokuwa na malengo ya udhibiti baada ya vikosi vya Nato kuondoka nchini humo 2014.
Ni mmoja wa viongozi wa kundi hilo ambaye amekuwa akipenda kufanyika kwa mazungumzo na Marekani pamoja na serikali ilioondolewa ya Afghanistan.Baada ya kuwa mmoja ya waanzislishi wa kundi la Taliban 1994, Mullah Baradar alijipatia kazi ya kuwa kamanda wa mikakati ya kijeshi.
Alidaiwa kusimamia operesheni za kila siku za kundi hilo na ufadhili wake.
Alisimamia majukumu muhimu katika vita vyote vikuu nchini Afghanistan, na kusalia kamanda mkuu wa kundi la Taliban katika eneo la magharibi la Herat pamoja na Kabul.
Wakati ambapo Taliban walifurushwa, alikuwa naibu waziri wa ulinzi. Mkewe ni dada yake Mullah Omar.
Alikuwa akifanya mashambulizi makali dhidi ya vikosi vya serikali ya Afghan , alisema afisa mmoja wa Afghan ambaye hakutaka jina lake litajwe wakati wa kukakamtwa kwake.
Mullah Baradar, kama viongozi wengine wa Taliban , alilengwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa , ambalo lilimshirikisha kupiga tanji mali ya kundi hilo, kulipiga marufuku kusafiri na kuzuia kundi hilo kuuziwa silaha.
Kabla ya kukamatwa kwake 2010, alitoa taarifa kadhaa kwa umma. Lakini mojawapo ya taarifa hizo ilikuwa 2009 mwezi Julai, ambapo alirushiana cheche za maneno la gazeti la Newsweek.