Colombia imetangaza kuwa wakimbizi wote wanaoishi nchini watapewa chanjo dhidi ya virusi vya corona.
Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Colombia, ilitangazwa kwamba wahamiaji nchini wametakiwa kujiandikisha kupigwa chanjo mpaka kufikia Agosti 30.
Ilielezwa kuwa kipaumbele kitapewa wajawazito na watu wazima katika chanjo, na kampeni ya kitaifa ya chanjo inaendelea kote nchini.
Kulingana na habari katika vyombo vya habari vya Colombia, inakadiriwa kuwa kuna karibu wahamiaji milioni 2 wasio wa kawaida nchini, wengi wao wakiwa wa Venezuela.
Colombia ni nchi ya tisa yenye idadi kubwa zaidi ya visa vya maambukizi ya corona ulimwenguni.