Malaysia. Msanii maarufu wa nchini Malaysia, Siti Sarah Raisuddin amefariki dunia kwa ugonjwa wa corona muda mfupi baada ya kujifungua.
Msanii huyo aliyejifungua akiwa na ujauzito wa miezi nane aliwekwa kwenye koma ili mtoto aweze kuzaliwa kwa njia ya upasuaji.
Mume wa msanii huyo ambaye anajihusisha na Sanaa ya vichekesho, Shuib Sepahtu amesema kuwa kabla ya umauti kumfika mkewe alifanikiwa kumpigia simu lakini kwa kuwa hakuwa akiweza kuzungumza machozi yalikuwa yakimtoka.
“Nina changamoto kubwa sana kuwaambia watoto wetu wengine watatu taarifa hizi za kifo cha mama yao.
Mbali na mtoto aliyezaliwa, wawili hao walifanikiwa kupata watoto wengine watatu wenye umri wa kati ya miaka tisa na 10