Shirika la ndege Delta, nchini Marekani linaazimia kuwapiga faini ya $200 (£145) kila mwezi wafanyakazi wake ambao hawajachanjwa dhidi Covid-19.
Pia iimesema kuwa tawalipia gharama ya matibabu ya Corona wafanyakazi ambao wamepewa chanjo kamili lakini wakaambukizwa ugonjwa huo.
Mkuu wa shirika hilo Ed Bastian amesema hatua hiyo itasaidia kudhibiti "maambukizi sugu' ya virusi vya corona ambayo yanaendelea kuongezeka kote nchini Marekani.
Hili ni jaribio la hivi punde la mashirikamakubwa kuwashurutishwa wafanyakazi kuchomwa chanjo ya corona.
Katika taarifa kwa wafanyakazi,Bw Bastian alisema faini ya Delta itaanza kutekelezwa kuangazia Novemba tarehe moja kwa wafanyakazi ambao wamejiunga na mpango wao wa bima ya afya kumaanisha wafanyakazi 75,000 wataathiriwa.
Amesema ugonjwa huo unagharimu $50,000 kwa kila mfanyakazi anayelazwa hospitali hali ambayo itaathiri shirika hilo kifedha siku zijazo.