Mwaka 1995 Toyota walipo leta Alteza sokoni maalumu kabisa kwajili yaku pambana na sport luxury sedan kutoka Ulaya.
Sifa ya sport luxury sedan ni lazima iwe ina handling nzuri kwenye kona, inafaa kusafiri nayo safar ndefu na mwisho inatakiwa iwe ina kimbia. Ya mwisho ndo ya msingi sana!!?
So kati ya hizi sifa Alteza ina ipi??
Kwanza kabisa engine zilizo kuja na alteza ilikua ni 1G, 3SFSE, 3SGT na 2JZ, hizo engines za mwanzo; 1G na 3S zilikua ni kituko kwasabau ata mtu akija na Peugeot 504 wewe upo na alteza anakupita and that can be depressing 😢. Alteza ilipata umarufu mkubwa kutokana na ubora wake, muonekano wake na how fun it was to drive thanks to Rear wheel drive alteza ni gari nzuri sana yaku chezea na kwasababu inashare parts nyingi na Aristo G ka alteza basically ni ka Ak47 kenye risasi zaki china. #wardogs
Tukija kufananisha na other luxury sport sedan kama 3series, C class kiukweli Alteza bado ipo nyuma sanaa.. lakini wajapan walificha jini moja na mtoto wake kwenye alteza 2jz, 3SGT na 1jz alteza zenye hizi engine ni balaa zinaitaji modification ndgo sana kuacha historia mahala popote na ni kwasababu alteza ni nyepesi so a small increase in power has a huge impact of how the car drives and handles which will leave a giant gap btn you and a 3series BMW .
Kama una Toyota alteza with 1G, 3S engines ni ngumu sana watu wanao jua magari kukuchukulia serious kwasababu kwenye macho yetu we unaendasha li Toy likubwaaa na kama unasoma hii review anza leo kufanya mabadiliko, tafuta alteza yenye engine yenye uwezo mkubwa. Utanishukuru ukifanikiwa otherwise msitupigie kelele na Fake exhaust sounds wakati Boxer yenye 150cc ina kushinda ku accelerate 🔥🔥🔥🔥.