Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu wamesomewa mashitaka sita ikiwemo la kutaka kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai wakati huo, Lengai Ole Sabaya.
Pia inadaiwa Freeman Mbowe alituma kiasi cha shilingi laki sita kwa Washitakiwa wenzake kwa ajili ya kufanya maandalizi ya vitendo vya Ugaidi ikiwemo kutaka kulipua vituo vya mafuta, mikusanyiko ya Watu, kukata miti na kuisambaza barabarani.
Mbali na Mbowe wengine kwenye kesi hiyo ni waliokuwa Walinzi wake, Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling'wenya ambapo wamesomewa mashitaka hayo leo Jumatatu, tarehe 23 Agosti 2021, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.
Mashtaka hayo ni pamoja na kula njama za kutenda ugaidi ambapo Mbowe anatuhumiwa kufadhili vitendo hivyo vya kulipua vituo vya mafuta kwa kutoa zaidi ya shilingi laki sita, pia Watuhumiwa wote wanatuhumiwa kushiriki vikao vya kutenda kosa la ugaidi huku Mshtakiwa wa pili anatuhumiwa kumiliki bastola yenye risasi tatu kwa ajili ya kutenda kosa la ugaidi huku Mshtakiwa wa kwanza akituhumiwa kumiliki nguo, begi na koti zote za Jeshi la Wananchi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Written and edited by @yasiningitu