Gwiji wa mpira afariki dunia kwa ugonjwa wa akili




Gwiji wa zamani wa mpira wa miguu wa Ujerumani Gerd Muller amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75, baada kusumbuliwa kwa takriban miaka sita na ugonjwa wa akili, klabu yake ya zamani Bayern Munich imetangaza.

Mshambuliaji huyo wa zamani ambaye alikuwa na jina la utani 'Der Bomber' alichukuliwa kama mmoja wa washambuliaji wakubwa kucheza mchezo wa soka na kuisaidia nchi yake kutwaa Kombe la Dunia la FIFA mwaka 1974 na taji la Euro mwaka 1972.

Muller pia aliweka rekodi ya kua mfungaji wa muda wote wa Bayern Munich akiwa na mabao 552 katika mechi 607 alizocheza, huku akiwa na jumla ya magoli 711 katika michezo 780 kwa ujumla wake katika muda wake wote akicheza soka katika ngazi ya kilabu na timu ya taifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad