Hakuna utafiti unaonesha chanjo ya Covid-19 ina madhara-Dk Janabi




Hakuna utafiti unaonesha chanjo ya Covid-19 ina madhara-Dk Janabi
MKURUGEZI wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi amewataka watu kuacha kutabiria chanjo ya Covid -19 kuwa ina madhara wakati hakuna utafiti uliofanyika kubaini hilo.

Prof Janabi aliyasema hayo Juzi wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) alisema hakuna madai ya kweli kuwa chanjo hizo zinasababisha matatizo ya uzazi au kugandisha damu.

“Najiuliza swali kubwa, hizi chanjo zimeanza kutolewa mwanzoni mwaka huu kwa sababu leseni zimetolewa Desemba 31 mwaka jana kwa chanjo zote hivyo sasa ni miezi saba tangu zianze kutolewa. Kwa hiyo hilo la uzazi linapozungumziwa, hawa watu wameshika ujauzito lini? Hata ingekuwa Januari bado hawajajifungua kwa hiyo ni sawa na kusema ngoja nifungue mwamvuli labda mvua itanyesha,” alisema.

Alisema wasiwasi kuhusu chanjo umekuwa mkubwa hali ambayo wataalamu wa afya wanatakiwa kutoa maelezo zaidi ili wananchi waelewe.

“Lakini hizi chanjo zimepita hatua mbalimbali, hatua ya kwanza zilikuwa 184 zikapunguzwa zikabakia 35 zikapunguzwa zikabaki 34,zikabaki 27 leo zinazotumika ni chanjo tisa. Hivyo Ingekuwa ni haraka, leo zingekuwa 100 kwa sababu tulianza na 184 katika majaribio ila leo ziko tisa hivyo wanavyosema imeenda haraka si kweli,”alifafanua.

Akizugunguza kuhusu kuganda kwa damu alisema “Mfano astrazenec walivyotoa dozi milioni moja, watu wanne walipata kuganda damu. Ukitazama kwa asilimia hiyo ni 0.004

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hizi akili mbovu hazitatusaidia kuna utafiti unaoonyesha kuwa Chanjo ya Covid-19 Ni salama?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad