Mtandao wa kijamii wa Facebook inachukulia Taliban kama kundi la kigaidi na hivyobasi, inapiga marufuku maudhui yote yanayounga mkono Taliban katika majukwaa yao.
Kampuni ya Facebook imesema timu ya wataalam wa Afghan inafuatilia na kuondoa maudhui yote yenye kufungamana na kundi hilo.
Facebook imegusia kwamba sera hiyo inatumika kwa majukwaa mengine yote ya mitandao yao ikiwemo Instagram and WhatsApp.
Hata hivyo, kuna taarifa kwamba Taliban inatumia jukwaa la mawasiliano la Whatsapp kuwasiliana.
Facebook imeiambia BBC kwamba itachukua hatua ikiwa itabaini akaunti kwenye programu za simu yenye kijihusisha na kundi hilo.
Majukwaa pinzani ya mitandao ya kijamii kama vile Twitter na Youtube pia nayo yameanza kufuatilia kwa karibu namna ya kushughulikia maudhui ya kundi la Taliban