IGP Sirro: Mbowe Sio Malaika, Ukiandamana Utakung’utwa




Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Simon Sirro amewataka wafuasi wa Chadema kuacha kuishinikiza mahakama ili Mwenyekiti wa chama hicho, Mhe. Freeman Mbowe aachiwe huru au kupewa dhamana.

 

IGP Sirro amesema hayo leo Jumatatu, Agosti 1, 2021 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam ku kuongeza kuwa tuhuma zinazomkabili Mhe. Mbowe ni za kweli.

 

“Niwaombe Watanzania tuache wale Watu wachache ambao wanataka kupambana na Serikali wapambane nayo labda wana sababu zake lakini Mtu wenye hekima na busara anielewe, lakini kikubwa kama wameandaa kwenda Canada au Marekani wajiandae ila hatuwezi kuruhusu Watu wachache wavuruge Nchi kwasababu wamekosa madaraka.

 

“Habari ya kusema mnataka kuandamana mnavunja sheria na ukivunja sheria usilaumu Jeshi, ukivunja sheria umeingia kwenye uhalifu, Sirro hatokuacha na Polisi hawatokuacha na ndio maana wanafanya siasa kwa sababu amani na utulivu upo, Sisi hatufanyi Siasa.

 

“Niwaombe Watanzania ambao wameambiwa mkusanyike kutoka Mara kutoka wapi sijui na muelewe Mahakamana ni kituo nyeti ni kama Kituo cha Polisi ukitaka kuvamia utakung’utwa kwa mujibu wa sheria sababu umetaka sasa kama kuna Mtu maisha yamemshinda aje ila asije kulalamika, hii kesi iko Mahakamani tuiachie Mahakama iamue,” amesema IGP Sirro.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad