Wakati klabu mbalimbali zikijiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara, Miamba ya soka nchini Yanga na Simba kila moja inajiandaa na safari ya kuelekea Morocco kama sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Young Africans Sports Club imesema kuwa wanajiandaa kwenda Morocco kwaajili ya maandalizi yao ya msimu.
”Kikosi cha timu ya Wananchi kitaondoka Dar es Salaam kwenda Morocco kwa Maandalizi ya msimu ujao.”- Taarifa ya Yanga.
Nao Simba dakika chache zilizopita Simba SC wametoa taarifa inayoeleza kuhusiana na safari yao nchini Morocco kama sehemu ya maandalizi.
”𝗠𝗼𝗿𝗼𝗰𝗰𝗼 ndio nchi ambayo mabingwa wa nchi tutaweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa 2021/22.” – Simba SC wakitoa taarifa yao
Wadau wengi wapenda soka wanaamini msimu ujao wa ligi 2021/22 utakuwa mgumu zaidi hasa kutokana na namna usajili wa ulivyofanyika hasa kwa klabu ya Yanga, Azam na hata ubora wa kikosi cha simba na hivyo kutakuwa na ushindani mkubwa.
Upi mtazamo wako, 2021/22 utakuwa msimu wa namna gani ?