Kenya na Uganda zashinda medali za kwanza za dhahabu katika mashindano ya Olimpiki



Emmanuel Korir ameishindia Kenya medali ya kwanza ya dhahabu katika mashindano yanayoendelea ya Olimpiki huko Japanbaada ya kushinda mbio za mita 800 na kumuongoza mkenya mwingine Ferguson Rotich kumaliza wa pili na kushinda nishani ya fedha .

Korir alimalizambio hizo kwa muda wa 1:45.06 kuhakikisha Kenya inasalia na taji hilo kwenye mbio hizo za mizunguko miwili ambazo David Rudisha alishinda miaka mitano iliyopita .Rotich alimaliza kwa muda 1:45.23 ili kushinda medali ya fedha .

Kwingineko katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi kwa upande wa akina dada mkenya Hyvin Kiyeng alimaliza wa tatu na kujishindia medali ya shaba . Mkenya huyo alimaliza kwa muda wa

9:05.39 katika mbio ambazo MgandaPeruth Chemutai alishinda dhahabualipotimka mita 300 za miwhso kumpita mmarekani

Courtney Frerichs ambaye alikuwa ameongoza katika raundi mbili lakini akalazimika kujishindia medali ya fedha.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad