Serikali ya Mexico ilifungua kesi dhidi ya watengezaji wakubwa wa silaha nchini Marekani kwa tuhuma za kusababisha vifo na kuchangia biashara haramu ya silaha.
Maafisa wanasema kwamba Mexico imedai fidia ya dola bilioni 10.
Kampuni hizo bado hazijatoa taarifa ya kesi iliyofunguliwa katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani.
Ripoti ya kesi hiyo ilijumuisha maelezo kwamba serikali ya Mexico inataka kumaliza mchakato ambao unarahisisha kikamilifu biashara haramu ya wauzaji wa dawa za kulevya na wahalifu wengine nchini.
"Watengenezaji wa silaha wanafahamu bidhaa zao zinatumika katika magendo na shughuli haramu dhidi ya raia wa Mexico na serikali." Ripoti ya hiyo ilieleza juu ya kesi iliyofunguliwa.
Kulingana na shirika la habari la Associated Press, serikali ya Mexico inakadiria kuwa karibu asilimia 70 ya silaha zilizosafirishwa nchini humo zinatoka Marekani. Ndani ya mwaka wa 2019 pekee, zaidi ya mauaji 17,000 yalihusishwa na silaha za magendo huko Mexico.