Kijana akamatwa akituhumiwa kuteka, kubaka watoto watatu Mtwara




Mtwara. Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia kijana Jabir Hamisi Bakari (19) kwa tuhuma ya kuteka, kubaka na kuwalawiti watoto watoto watatu.
Kijana huyo ambaye anadaiwa kutokuwa na kazi wala makazi maalumu ambaye alikamatwa Agosti 12, 2021 hupendelea kushinda maeneo ya Mbae akiwarubuni watoto na kufanikiwa kuondoka nao kwenda kwenye maeneo mengine ambako huanzisha makazi ya muda akiwa na watoto hao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Marc Njera amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema katika tukio la kwanza Juni 25 mwaka huu maeneo ya Mbae Mashariki mtuhumiwa alienda kwenye eneo wanapocheza kundi la watoto na kufanikiwa kumchukua mtoto mwenye umri wa miaka 8 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili na kwenda kuishi naye karibu siku nne baada ya kumlaghai kwenda kumnunulia pipi na kumpa fedha.

Kamanda Njera amesema tukio hilo liliporipotiwa Polisi lilifatilia na kufanikiwa kumpata mtoto akiwa amefanyiwa vitendo vya ukatili Vya ubakaji.


 
Katika tukio la pili, Kamanda Njera amesema lilitokea Julai 8 katika eneo hilo ambapo mtoto wa kike mwenye miaka 7 alitoweka nyumbani kwao akiaga kuwa anakwenda shule na taarifa za kupotea kwake zilichelewa kuripotowa.

“Baada ya taarifa hiyo kuripotiwa jeshi la polisi lilifanikiwa kumpata mtoto huyo Julai 24, mwaka huu na katika mahojiano alieleza wazi kwamba kuna mtu alimlaghai anaenda kumnunulia pipi kisha atampa fedha za matumizi lakini alipoondoka naye alimpeleka kwenye kichaka karibu na shule ya Sekondari ya Aquinas akakaa naye karibu siku kumi akimfanyia vitendo vya udhalilishaji” amesema Kamanda Njera

Ameeleza kuwa walipokua wakifatilia mtuhumiwa alimwacha mtoto kisha akakimbilia katika mahojiano mtoto alieleza wajihi wa mtuhumiwa na wakati anafatiliwa alikimbilia Songea.


“Alirudi baadaye na Agosti 6 mwaka huu alimchukua mtoto mwengine mwenye umri wa miaka 9 akampeleka kwenye kichaka na kumfanyia vitendo vya udhalilishaji” amesema Kamanda Njera na kuongeza

“Agosti 12 mwaka huu mtuhumiwa alikamatwa kwa usaidizi wa wananchi na alikiri kuhusika na matukio yote matatu”.

Kamanda Njera amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi muda wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

"Natoa onyo kali kwa wale wote wanaojihusisha na udhalilishaji na masuala ya ukatili kwa watoto waache mara moja hawana nafasi tena na atakayebainika tutachukua hatua kali dhidi yake" amesema Kamanda Njera

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad