Waziri wa elimu wa Uganda ameamuru walimu nchini kote kupata chanjo ya Covid-19 vinginevyo wazuiwe kuingia madarasani shule zitakapofunguliwa.
Janet Museveni, ambaye ni mke wa Rais Museveni, ameonya kuwa mwalimu yeyote atakayekwenda kazini akiwa na cheti cha kughushi kuthibitisha kuwa amechanjwa atakuwa hatarini kupoteza kazi yake.
Amesema kuchanjwa kwa walimu kutasaidia kuwalinda wanafunzi dhidi ya virusi na kuongeza kuwa vituo vya chanjo vitawekwa kwenye shule na vyuo vikuu vitakapofunguliwa.
Bibi Museveni amekuwa kwenye shinikizo wiki za hivi karibuni la kutakiwa kufugua tena shule, ambazo zilifungwa tarehe 6 mwezi Juni ili kudhibiti maambukizi ya wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona.