Maandamano mapya yazuka Ufaransa kupinga kibali cha kiafya cha Macron





Waandamanaji wameingia mitaani leo kote Ufaransa katika wikendi ya nne mfululizo kuadamana dhidi ya kibali kipya cha afya cha virusi vya corona kinachohitajika ili kuingia mgahawani au kusafiri kwenye treni za kutoka mji mmoja hadi mwingine. 
Maandamano ya leo yamekuja ikiwa ni siku mbili kabla ya sheria hizo mpya kuanza kutekelezwa. Sheria hizo zinazoungwa mkono na Rais Emmanuel Macron zinahitaji ama kibali cha dozi kamili ya chanjo ya Covid-19, kuwa na umiliki wa cheti cha kinachoonesha mhusika hana mambukizi au kapona katika siku za karibuni kutokana na virusi hivyo ili kufurahia shughuli za kawaida za nje. 

Macron, ambaye anatafuta kuchaguliwa tena mwaka ujao, anatumai sheria hizo mpya zitawahimiza Wafaransa wote kuchanjwa dhidi ya Covid-19 na kukiangamiza aina ya kirusi kipya kinachosambaa kwa kasi cha Delta. 

 Lakini wapinzani wanaofanya maandamano wanahoji kuwa sheria hizo zinakiuka haki za kiraia katika nchi ambayo uhuru wa mtu binafsi unaheshimika mno

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad