Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge pamoja na wajumbe wa kamati ya usalama ya wilaya ya Rufiji wamefika kwenye tukio la moto lililotokea usiku wa kuamkia leo ili kuona atahari iliyotokea na jitihada ambazo uongozi wa wilaya wamezichukua kuhakikisha wananchi wanakuwa salama katika kitongoji cha Shaurimoyo kijiji cha Nyamwage Kata ya Mbwara ambapo nyumba zaidi 19 zimeteketea mara baada ya mwananchi mmoja akiwa anasafisha eneo lake moto ulimshinda na kuteketeza nyumba zipatazo 19 za wananchi pamoja na mali na thamani zilizopo ndani ya nyumba hizo na hakuna majeruhi yoyote katika ajali hiyo.
Aidha Abubakari Kunenge ametoa pole kwa serikali ya wilaya pamoja na wananchi waliokutwa na madhira hayo na kuwapongeza wakazi wa maeneo ya karibu kuweza kuwapatia hifadhi wananchi wenzao waliokutwa na ajali hiyo na kuwaagiza uongozi wa wilaya hiyo kufanya haraka kujua tathmini ya athari iliyopatikana ili kuweza kuwasaidia waliopata ajali hiyo...Insert Abubakari Kunenge.
Kwa upande wake Mkuu wa wailaya ya Rufiji Meja Edward Gowele ameeleza kama wilaya hatua walizochukua mara baada ya kutokea tukio hilo na kutoa rai kwa wakazi wa wilaya hiyo kuw a makini wakati wanachoma moto kwani kwa sasa ni kipindi cha upep mkali..Meja Edward Gowele.
Wananchi wa eneo hilo nao wameeleza tukio jinsi lilivyowaathiri hivyo kuomba serikali kuweza kuwasaidia kwa haraka maana hawana mahala pakuishi...Insert Wakazi wa Rufiji