Majenerali Waliopanga Kumuua Rais wa Madagascar Wakamatwa





MAOFISA wa kijeshi wa ngazi ya juu na polisi wamekamatwa nchini Madagascar kuhusiana na jaribio la kumuua rais lililotibuka. Waliokamatwa ni pamoja na majenerali watano na maafisa kadhaa wa polisi na kufikisha 21 jumla ya watu ambao wanachunguzwa ufuatia tukio hilo a mwezi uliopita.

 

Mamlaka pia imepata bunduki moja na dola 250,000 za Kimarekani, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti. Jaribio la kumuua Rais Andry Rajoelina ni sehemu ya misukosoko ambayo imekuwa ikikumba taifa hilo la kisiwani.

 

Miongoni mwa waliokamatwa karibuni walikuwa 12 “wanajeshi na polisi wanaofanya kazi, ikiwa ni pamoja na majenerali watano, manahodha wawili na maafisa watano ambao hawajapewa kazi”, Mwanasheria Mkuu Berthine Razafiarivony alisema.

 

Madagascar imekuwa ikitekeleza amri ya kutotoka nje tangu janga la Covid-19 lilipozuka mwaka jana huku sehemu ya kusini mwa nchi hiyo ikikabiliwa na hatari ya kukumbwa na baa la njaa. Rajoelina, 47, alichukua madaraka mnamo 2009 kutoka kwa Marc Ravalomanana akiungwa mkono na jeshi.

 

Rajoelina aliapishwa kama rais wa nchi ya kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi mnamo 2019 baada ya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali na ambao ushindi wake ulipingwa katika mahakama ya kikatiba na mpinzani wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad