Majeruhi wa tukio la shambulio la silaha wafanyiwa upasuaji, wawili waruhusiwa





Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipokea majeruhi watano jana tarehe 25 Agosti, 2021, kuanzia majira ya saa saba mchana wakiwa na majeraha makubwa na wengine madogo sehemu mbalimbali za miili yao ambapo wanne kati yao ni Askari wa Jeshi la Polisi na mmoja ni Mlinzi wa kampuni binafsi ya SGA.
 
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ya umma Hospitali ya Taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha amesema, Mara tu baada ya kupokelewa, askari wawili ( miaka 41 &  miaka 49) walikua na majeraha makubwa   katika sehemu  mbalimbali za Mwili na ya viungo vya ndani hivyo kufanyiwa upasuaji wa haraka ambapo upasuaji ulienda vizuri.
 
Askari wa tatu (miaka 35) naye alipata majeraha mbalimbali  makubwa na madogo  katika maeneo ya    mikono na mgongoni ambaye alipewa huduma stahiki na kufungwa vidonda.
 
Askari wa nne (miaka 46), alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani  kwakua alikua na majeraha madogo. 
 
Mlinzi wa SGA (miaka 42) naye alikuwa na majeraha ambayo hayakuhitaji upasuaji hata hivyo alilazwa wodini jana na ameruhusiwa leo kwenda nyumbani kuendelea na matibabu akiwa nyumbani
 
Hivyo, tumebakiwa na majeruhi watatu ambao wanaendelea kupata matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika.
 
Hata hivyo tulipokea mwili wa marehemu mmoja   kutoka kwenye tukio hilo ambaye alikuwa ni Mlinzi wa SGA na mwili wake umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti.
 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad