Maskini Simba Kwisha Habari yake..CLATOUS Chama Atimka na Kusajiliwa na Timu hii ya Morocco



CLATOUS Chama kiungo namba moja kwa kutengeneza pasi za mwisho usiku wa kuamkia leo Agosti 13, 2021 ametajwa kujiunga na Klabu ya RS Berkane ya Morocco kwa dili la miaka mitatu.


Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge ambaye alikuwa anafundisha AS Vita anatambua vema uwezo wa Chama kwa kuwa alikutana naye kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.


Ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 nyota huyo alitengeneza jumla ya pasi 15 na alifunga mabao nane akiwa ni namba moja kwa utengenezaji wa pasi ndani ya ligi.



Taarifa zimeeleza kiungo huyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao wa 2021/22.

Mbali na Chama pia nyota wao Luis Miquissone yupo kwenye hesabu za mwisho kutua nchini Misri kwa ajili ya kujiunga na Klabu ya Al Ahly ya Misri.


Tayari jezi namba 11 ambayo aliyokuwa anavaa Luis amekabidhiwa kiungo mpya Peter Banda ambaye anatajwa kuwa mbadala wa nyota huyo.


Simba imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22 ambapo Luis hakuwa sehemu ya kikosi hicho ambacho kipo kambini.


Simba kuwauza mastaa wake wawili tegemeo, Luis Jose Miquissone na Clatous Chama imekuwa gumzo kwa wachambuzi na mashabiki wa mpira wameonekana kushtushwa na uamuzi huo.

Lakini mitandao mingi imefichua kwamba biashara waliyoifanya Simba ni ya kiwango cha juu kwa klabu inayoanza kukua kibiashara.


DROO YA SIMBA, YANGA

Droo ya michuano ya kimataifa itakayotoa washindani wa Simba, Yanga, Azam na Biashara itachezeshwa leo Ijumaa jijini Cairo kwa mujibu wa Caf.

Timu kumi bora ambazo hazitaanzia katika hatua ya awali kwenye ligi ya mabingwa Barani Afrika msimu huu.

1. Al Ahly 2. Zamalek 3. Espérance 4. ES Sahel 5. Wydad Casablanca 6. Raja Casablanca 7. TP Mazembe 8. Mamelodi Sundowns 9. Horoya AC 10. Simba SC

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad