Mshambuliaji nyota wa Argentina Leonel Messi hatimaye ametangaza rasmi kuondoka kwake klabu ya Barcelona baada ya kuichezea kwa takriban miaka 21.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Jumapili katika uwanja wa Nou Camp Messi aliyeshindwa kujizuia aliangua kilio na wakati alipokuwa akiaga klabu hiyo.
"Familia yangu na mimi tuliamini kuwa tutakaa hapa nyumbani, ndivyo sote tulitaka zaidi ya kitu chochote.
"Tulifanya hapa kuwa nyumbani na tulifikiri tutaishi Barcelona.
"Wakati ambao nimekuwa nao hapa umekuwa mzuri usiokuwa na kifani lakini leo lazima nisema kwaheri. Nimekuwa hapa miaka mingi sana, maisha yangu yote tangu nilipokuwa na miaka 13. "
Tayari Lionel Messi na Paris St-Germain wamekubaliana mkataba wa miaka miwili, huku mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 34.
"Ningelipendelea kushinda taji lingine la Ligi ya Mabingwa, naamini tungeliweza kushinda tena kwa maoni yangu '' aliendelea kusema.
Pia alizungumzia uhusiano wake na Barcelona akisema: "Nilijitolea kupunguza mshahara wangu kwa 50%, lakini hawakuniuliza kitu kingine chochote. Habari nilizoomba 30% zaidi ni uwongo, mambo mengi ambayo watu wanasema sio kweli."
Kuondoka kwa Lionel Messi sio pigo tu kwa Barcelona, pia ni pigo kwa La Liga, ambayo imepoteza mfungaji mabao wake hodari.
Gazeti la Ufaransa la L'Equipe linaripoti kuwa Messi atafanyiwa uchunguz wa kimatibabu mjini Paris Saint-Germain Jumapili usiku au Jumatatu asubuhi.