Mfungwa mmoja Shane Goldsby ( 26 ) ameongezewa kifungo cha miaka ishirini na tano gerezani baada ya kumuua mfungwa mwenzake baada ya kugundua aliingia gerezani humo kwa kumbaka dada yake.
Mfungwa huyo Goldsby raia wa Marekani katika jiji la Washington anadaiwa kumuua Robert Munger (70) ambaye aliingia gerezani mwaka 2019 akitumikia kifungo cha miaka 43 kwa kukutwa na hatia ya kumbaka msichana mdogo.
Wafungwa hao wakiwa katika gereza la Airway Heights Corrections Center hukohuko Washington inadaiwa Goldsby (muuaji) alikuwa amefungiwa katika chumba kimoja na Munger ( aliyeuawa) kabla ya kumvamimia na kukipiga kichwa chake katika ukuta kabla ya askari kuja kutoa usaidizi na kumkibiza hospitali Munger kwa matibabu.
Siku tatu baadaye mfungwa huyo Munger alifariki dunia mnamo mwezi June 2020 kutokana na athari zilizotokana na kupigwa kichwa ukutani.
Mfungwa Shane Goldsby ( muuaji) aliingia gerezani mwaka 2017 baada ya kupatikana na hatia ya gari la doria huko Washington na kumjeruhi askari wakati akitaka kumkamata .
Kijana huyo baada ya tukio hilo na kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha miezi tisa gerezani ambako sasa atalazimika kuka zaidi ya miaka ishirini na tano baada ya kupatikana na hatia ya mauaji.
Uongozi wa gereza kulimotokea mauaji ,umesema haukuwa na taarifa zozote kama wafungwa hao wawili walikuwa wakifahamiana na walikuwa na kisasi na waliamini walikuwa ni wafungwa kama wafungwa wengine tu.