MREMBO Mkenya ameibua hisia mseto mitandaoni baada ya kusimulia namna alikutana na baba yake kwa mara ya kwanza kupitia Facebook.
Getrude Wanjiru alifichua kwamba hakuwa anamfahamu baba yake kwa miaka 27, hadi alipomtafuta kwenye Facebook. Akizungumza katika mahojiano na NTV, Wanjiru alisema alilelewa na babu na bibi yake.
”Mama yangu alinizaa na kunipeleka kwa wazazi wake,” Getrude alisema. Getrude alisema hakuwa na hamu ya kumtafuta baba yake kwa sababu babu yake alikuwa amejitwika wajibu huo.
“Sikushughulika kumtafuta baba yangu kwa sababu alikuwa babu yangu alikuwa kama baba kwangu na alinipa chochote nilichokuwa nataka,” alisema Ilikuwa baada ya kifo cha babu akiwa katika chuo kikuu ndipo aliamua kumtafuta baba yake kujaza pengo hilo.
Hofu ya kuchumbiana na jamaa wake Alisisitiza kuwa alikuwa anahofia kuingia katika mahusiano ya kimapenzi akiwa na hofu kuwa huenda atachumbiana na baba yake ama kaka zake bila kujua na hivyo alimshinikiza mama yake amuonyeshe baba yake.
Hatimaye mwaka 2019, mama yake aliamua kumuambia kumhusu baba yake pamoja na jina lake japo hakuwa na nambari zake za simu. Hivyo Getrude aliamua kufanya utafiti wa kumsaka baba yake.
Msako wake ulianzia Facebook, na kwa bahati nzuri alimpata baba yake na mama yake alimthibitishia kuwa kweli jamaa huyo alikuwa baba yake mzazi. Hata hivyo, mzee huyo mara ya kwanza alikataa kuamini lakini hatimaye alichukuwa hatua ambayo ilimfurahisha Getrude. Getrude alisema alifurahi wakati baba yake aliwasiliana naye na hatan kupanga wakutane.