Msaidizi wa rais wa Malawi akamatwa kwa shutuma za matumizi mabaya ya ofisi





Polisi nchini Malawi inawashikilia watu wawili, akiwemo msaidizi wa Rais Lazarus Chakwera,kwa kupeleka muswada bungeni ambao ungetoa fursa kwa matumizi ya serikali bila kufuata taratibu.
Gazeti linaloongoza nchini humo, The Nation, limeripoti kuwa muswada huo ulianzia Ikulu ulikua ukitafuta idhini ya kukopa kiasi cha dola za kimarekani milioni 116 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za polizi, jeshi na idara ya uhamiaji.

Lakini Nation limesema muswada huo ulipelekwa bungeni bila baraza la mawaziri kufahamu na taasisi nyingine zinazohusika.

 mebainika kuwa msaidizi huyo muhimu wa rais , Pastor Thom Martin, amekuwa akishutumiwa kuhusika na mpango wa kupeleka muswada huo.

Baada ya saa chache tangu kukamatwa kwake Rais Chakwera alitoa taarifa ya kumfukuza kazi Bw. Martin.

Hakuna taarifa yoyote kutoka kwa Bw. Martin, lakini polisi wamesema kuwa atashtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya ofisi na kuwa atafikishwa mahakamani hivi karibuni.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad