Mtu aliyepatikana na viungo vya binadamu kwenye jokofu akamatwa




Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 28 anashikiliwa na polisi kwa mauaji mkoa wa Bono.
Polisi nchini Ghana wanachunguza mauaji ya watu watatu ambayo yanaonekana kuwa mauaji ya mfululizo.

Mshukiwa wa mauaji hayo alikamatwa Ijumaa katika eneo la Bono.

Idara ya polisi Ghana imesema kwamba imemkamata mshukiwa huyo kwa madai ya mauaji ya watu watatu wenye umri wa miaka 12 na 15 na mwingine ambaye bado wanajaribu kumbaini.

Tukio hilo limezua wasiwasi miongoni mwa raia kwasababu linawakumbusha wasichana wa Takoradi wasiojulikana walipo ambalo limetokea hivi karibuni.

Polisi walitoa taarifa wakisema kwamba kukamatwa kwa mshukiwa kumetokea baada ya kufanyika kwa msako. "Polisi kwa ushirikiano na jamii imefanikiwa kumkamata mshukiwa mmoja kwa jina Richard Appiah ambaye inasemekana anasaidia katika uchunguzi".

Hayo ni kulingana na taarifa ya kamishna msaidizi wa polisi Kwesi Ofori.

Uchunguzi uliofanywa unaonesha kwamba mshukiwa alimdanganya mvulana wa miaka 12 kutoka kwenye uwanja wa kucheza mpira na kumpeleka hadi kwenye chumba chake kabla ya kumuua.

Baada ya baba wa kijana huyo kumtafuta mwanae hadi jioni saa kumi na moja na dakika 40, kukaanza kusambaa taarifa kwamba wa mwisho kuonekana na kijana huyo alikuwa Appiah.

Na baada ya polisi kufuatilia taarifa hiyo, walibaini viungo vya mwili wa binadamu vikiwa vimehifadhiwa kwenye jokofu pamoja na vichwa vingine vitatu vya binadamu, kulingana na taarifa ya polisi.

Mwili wa kijana huyo mdogo ulikuwa umelala chini kwenye sakafu. Kulingana na walioshuhudia mkasa huo, shughuli zaidi za kupekua chumba cha anayedaiwa kuwa muuaji zimeonesha kwamba kulipatikana mwili wa mwanadamu uliokuwa kando na vichwa vya binadamu ndani ya chumba chake.

Kwa sasa hivi, Appiah anasaidia polisi katika uchunguzi kubaini chanzo cha mauaji ya watu hao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad