Mwenyekiti wa Kitongoji Ambaka Shemeji yake

 


Mwenyekiti wa kitongoji cha Kanami, katika kijiji cha Isangijo wilayani Magu mkoani Mwanza Robert Mfungo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia maumivu makali binti wa miaka 12 ambaye pia ni shemeji yake.

Tukio hilo la kubakwa binti huyo limetokea majira ya jioni siku ya tarehe 2 mwezi huu nyumbani kwa Mwenyekiti, huyo ambapo anaishi na binti huyo ambaye ni mdogo wa mke wake wa pili.

EATV imekutana na majirani na wanadai tukio hili siyo la kwanza kufanywa na Mwenyekiti huyo huku wakidai kuwa Mwenyekiti huyo hastahili kuwa na wadhifa huo kutokana na matendo yake yasiyofaa kwa jamii.

“Nimefanya utafiti pale hospitalini ikasemakana kuwa mtoto amekiri kuwa alipewa maziwa na alimchukua, anatudhalisha wanawake na chama hii ni kesi ya pili kwake halafu kesi za kuwapa wanafunzi ujauzito na kuwakatisha masomo ni nyingi sana,” amedai Katibu wa CCM tawi la Isangijo Neema Kabote.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isangijo Malimi Pombe amesema kwa mujibu wa maelezo ya hospitali wamethibitisha mtoto kufanyiwa kitendo hicho.

Naye mke mkubwa wamtuhimiwa Bi. Vumulia Charles amesema wamejaribu kufuatilia lakini walipouliza mlengwa alikataa huku mhanga wa kitendo hicho akidai kuwa amakuwa anachanganya maneno hivyo kutokueleweka.

Akizungumza kwa sharti la kutorekodiwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi amesema Mwenyekiti huyo anashikiliwa kwenye kituo cha Polisi Magu kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo la ubakaji.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad