Ndoto ya Hamza kujenga shule yaacha simanzi Chunya


Mbeya. Wakati bado kukiwa na majonzi ya vifo vya askari polisi waliokuwa wakipambana na mfanyabiashara wa madini, Hamza Mohamed ambaye pia aliuawa, baadhi ya wananchi wilayani Chunya mkoani wameeleza ndoto ya mfanyabiashara huyo kuwajengea vyumba viwili vya madarasa ya awali mwaka huu katika eneo alilokuwa akiishi.


Mauaji hayo yaliyotokea Agosti 25, 2021 karibu na ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, baada ya Hamza kuwashambulia askari watatu kwa risasi mlinzi wa kampuni ya GSA, kabla na yeye kuuawa na askari wengine.


Ndoto hiyo ya marehemu Hamza imeelezwa kuwa ni kidonda na machungu kwa wananchi waliokuwa wakiishi naye kitongoji cha Kitete kilichopo kata ya Bwawani wilayani ambapo mfanyabiashara huyo alikuwa na mgodi wa madini ya dhahabu.


Diwani wa Kata ya Bwawani ambako alikuwa akiishi, marehemu Hamza amesema hilo ni pigo kwani alikuwa na ndoto za kuleta mabadiliko makubwa.


"Huyo kijana kwa kweli ametuumiza sana kwani alikuwa ni mtu wa kujitolea kwenye mambo mengi ya maendeleo pamoja na kujenga ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa gharama zake mwenyewe na mambo mengine mengi kwa jamii"amesema.

Ameongeza; "Alipanga mwaka huu kutekeleza ndoto yake ya kujenga shule kwa kianzia vyumba viwili vya madarasa ya chekechea endapo biashara ya madini ingeenda vizuri lengo kuwezesha watoto walio na umri wa kwenda shule wapate elimu bure ndoto ambao imezima na kugeuka maumivu," amesema.

Naye Eva Said kazi wa kitongoji hicho, amesema kuwa marehemu Hamza ameacha maumivu makali kwao kwani lengo lake la kujenga shule lingekuwa chachu kwa watoto kupata elimu na kwamba alihaidi kukibatilisha kitongoji chetu ambapo kwa bahati mbaya amekatishwa uhai wake akiwa bado na ndoto za kuisadia jamii.


"Kwa kweli tumeumia sana kwani tulimpenda kutokana na jinsi alivyokuwa akijitoa na kusaidia wananchi,miradi ya maendeleo kwa kweli ni pigo kubwa sana kwetu wananchi ambao tulikuwa tukiishi naye," amesema.


Mfanyabishara katika Mamlaka ya mji wa Makongorosi , Lawena Nsonda  amesema kuwa kimsingi marehemu alikuwa  ni mtu anayejishusha na kuongea na kila mmoja ikiwa ni pamoja na kuchangia maendeleo na alifahamiana naye wakati akijenga Ofisi cha Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani alikuwa akimuungisha vifaa vya ujenzi.


Mwenyekiti wa wachimbaji wa madini Wilaya ya Chunya, George Mtashi amesema kuwa kifo cha Hamza kimewaumza sana kutokana na mchango wake mkubwa kwa jamii na ndoto alizokuwa nazo wilayani humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad