Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi kwa kutumia silaha aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya ameanza kutoa utetezi wake jana katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha .
Akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi Odira Amworo akiongozwa na wakili wake Moses Mauna mstakiwa huyo Lengai Ole Sabaya ameielezea mahakama kuwa mnamo tarehe tisa mwezi wa pili 2021 alikuwa Bomang'ombe makao makuu ya wilaya ya Hai na alikuwa anaongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuanzia asubuhi saa tatu na nusu hadi saa nane na nusu mchana.
Sabaya amesema kuwa baada ya kumaliza kikao hicho saa nane mchana hadi saa tisa kasoro alipokea maelekezo na mamlaka za uteuzi ikamtaarifu kuwa kuna watu wameshuka Uwanja wa Ndege wa KIA na alipaswa kuwachukua na kuambatana nao kwaa ajili ya kuwafikisha mkoani Arusha.
Ndipo baada ya hapo aliwatafutia gari huku akiwa na gari lake binafsi ambalo alikuwa anaendeshwa na dereva wake huku jumla wakawa na magari mawili nakuanza safari kwenda Arusha huku aliokuwa amewachukua walikuwa na taarifa walichoagizwa huko Arusha.
Amesema mahakamani kuwa ilipofika saa saa kumi na moja na dakika arobaini na tano jioni walifika Arusha baada ya kufika walienda eneo ambalo walielekezwa kwa ajili ya kufanya mahojiano na muhusika ambae ni mmliki wa duka la shahidi Store Muhamed Saad lakini hakumkuta.
amesema baada ya kumkosa mmiliki huyo licha ya watu hao waliongozana nao ambao hakuwataja mahakamani hapo na kudai hawahusiki na shitaka hilo walikuwa na taarifa zote kwamba watamkuta mmiliki huyo.
Sabaya amesema kuwa baada ya kumkosa mmiliki huyo alifanya mawasiliano na mamlaka waliopewa maelekezo hayo kisha ikawaambia kuwa wameshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha hivyo hao watu waliowakuta katika duka hilo wapelekwe kituo cha polisi kwa sababa watasaidia kupatikana kwa muhusika na yeye akaelekezwa kuwasiliana nae huyo mkuu wa wilaya.
Akaeielezea mahakama kuwa mshtakiwa wa pili Silvesta Nyegu hakuwepo katika tukio hilo na mshtakiwa wa tatu Daniele Mbura hamfahamu kabisa na wala hajawahi kuonana nae maisha yake yote .
Amesema kuwa Bakari Msangi hakupigwa kama anavyodai na alichokielezea mahakamani hapo ni uongo na yeye hamfahamu kama amepigwa na kwamba Bakari Msangi ameamua kufanya hivyo kutokana na ugomvi wa kisiasa wa muda mrefu baina yake na yeye baada ya kumshinda katika uchaguzi wa kiti uwenyekiti wa umoja wa wavijana chama cha mapinduzi yeye pamoja na wenzake.
Hakimu mkazi Mwandamizi Odira Amworo ameahirisha kesi mpaka Jumatatu tarehe 16 Agosti 2021 ambapo mshatakiwa huyo ataendelea kutoa utetezi wake.