Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro, wanatarajia kuwa mashahidi kwenye kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Mbowe na wenzake watatu kwa sasa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kudaiwa kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.Mwananchi limeripoti
Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi namba 63/2020, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hayo yameelezwa leo, Agosti 23, 2021 na wakili wa washtakiwa hao, Peter Kibatala, baada ya upande wa mashtaka kumaliza kuwasomewa washtakiwa hao, maelezo ya mashahidi, idadi ya mashaidi na idadi ya vielelezo.
Katika ukurasa wake wa twitter Chadema imesema;
Wakili Kibatala ameiomba Mahakama imlete IGP Sirro na Ole Sabaya mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hiyo.
Kesi hiyo itasikilizwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
A