Olimpiki Tokyo 2020: Mganda Joshua Cheptegei ashinda dhahabu katika mbio za mita 5,000





Joshua Cheptegei wa Uganda alishinda medali yake ya pili kwenye Olimpiki ya Tokyo wakati aliponyakua dhahabu ya mbio za 5,000m ili kuiongeza na medali ya fedha alioshinda katika mbio za mita 10,000.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 24 alimaliza mbele ya Mzaliwa wa Somalia raia wa Canada Mohammed Ahmed, ambaye alishinda fedha, na mzaliwa wa Kenya Mmarekani Paul Chelimo, ambaye alichukua shaba kuiunganisha na fedha yake kutoka Michezo ya Rio.

Cheptegei anakuwa raia wa kwanza wa Uganda katika historia kushinda medali mbili za Olimpiki baada ya kushinda fedha katika mita 10,000 za wanaume wiki moja iliyopita.

Chelimo wa Marekani alijirusha utepeni kumnyima Mkenya Nicholas Kipkorir Kimemi medali ya shaba .

Jacob Kiplimo wa Uganda, ambaye alikuwa mshindi wa medali ya shaba katika mita 10,000, alikuwa wa tano na mwenzake Oscar Chelimo alimaliza katika nafasi ya mwisho wakati Milkesa Mengesha wa Ethiopia alikuwa wa 10.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad