Rais wa Marekani, Joe Biden amesema hakuna Mmarekani atakayeachwa Afghanistan




Rais Joe Biden amesema wanajeshi wa Marekani wanaweza kukaa Afghanistan zaidi ya tarehe ya mwisho ya kujiondoa, wakati wapiganaji wa Taliban wenye silaha wakiwaweka raia wake katika hofu ya kufika uwanja wa ndege wa Kabul.
Bwana Biden anataka vikosi vya Marekani viondoke mwishoni mwa mwezi Agosti, lakini hadi sasa raia 15,000 wa Marekani wamekwama nchini humo.

Rais wa Marekani aliiambia ABC News machafuko huko Kabul hayakuepukika.

Serikali za kigeni zinazidisha safari za ndege kwa ajili ya raia wa magharibi na Waafghan ambao walifanya kazi nao.

Karibu wanajeshi 4,500 wa Marekani wanadhibiti kwa muda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Karzai katika mji mkuu wa taifa hilo, lakini wapiganaji wa Taliban na vizuizi vya ukaguzi vinazunguka eneo hilo.

Taliban wanawazuia Waafghan wasio na hati za kusafiri - lakini hata wale walio na idhini halali wamepata taabu.

Mkalimani mmoja wa Afghanistan aliripotiwa kupigwa risasi ya mguu na Taliban alipojaribu kufika uwanja wa ndege Jumanne usiku kwa ajili ya kupanda ndege ya kuwaokoa wanajeshi wa Australia.

Picha zilizochapishwa na SBS zilimuonesha mtu huyo akitibiwa jeraha la risasi na daktari. Raia wengine wa Marekani waliwaambia washirika wa BBC, CBS News pia hawakuweza kuingia kwa ndege zilizopangwa za uokoaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad