Rasmi, Chama Awaaga Mashabiki Wake Na Viongozi "Ngumu Kuamini Baraka Mpeja Hatonitaji Tena Msimu Ujao"




CLATOUS Chama nyota wa Simba leo ameaga rasmi kwa mashabiki pamoja na viongozi wa Simba kwa kumaliza na neno moja kwamba, ‘Asanteni Sana’.


Ni rasmi kwamba kiungo huyo mshambuliaji kipenzi cha mashabiki na chaguo la kwanza la makocha wote waliopita ndani ya Simba ikiwa ni pamoja na Patrcik Aussems, Sven Vandenbroeck na hata huyu wa sasa Didier Gomes hatakuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22.


Akiwa na miaka 30 anakwenda kupata changamoto mpya na habari zinaeleza kwamba anakwenda RS Berkane ya Morocco na kila kitu kimekamilika.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chama amesema:-“Nimekuwa kimya kwa muda tangu mara ya mwisho nitume ujumbe wowote kwenye kurasa zangu za kijamii, ilibidi iwe hivyo kwa sababu kuna mambo nilikuwa ninakamilisha na nilikuwa nasubiri taratibu zote zikamilike. Siwezi kuwaacha nyinyi kwenye giza.


“Stori yangu ilianza pale nilipokuja Tanzania 2018, sikuwa najua kwamba ningeweza kuwapata watu wengi, kuweza kuongea kiswahili lakini upendo ambao nimeweza kuupata hapa hauelezeki katika maisha yangu.


“Siwezi kueleza namna ninavyohisi kuhusu Simba, kwa maneno machache ni kwamba bado ni ngumu kuamini kwamba jina langu halitatajwa na Baraka Mpenja msimu ujao ama sitavaa jezi yangu namba 17 katika timu ambayo ilikuwa ni ya nyumbani.


“Asante kwa viongozi wa Simba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mr Mo Dewji, CEO, Barbara Gonzalez, uongozi wa timu kiujumla, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenzagu pendwa asanteni kwa upendo wenu.


“Kwa mashabiki nitazidi kuwakumbuka nasema asante sana nitazidi kuwasiliana nanyi kupitia mitandao ya kijamii, nitaendelea kushangilia pamoja nanyi labda ikitokea nikacheza nanyi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa heri na asanteni” .

“Asanteni Sana’.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad