Msanii wa Bongo Fleva, Recho amesema sababu kubwa ya kutowahi kumuweka mpenzi wake hadharani kwa miaka yote tangu amekuwa maarufu kwenye muziki, ni kuhofiwa kuibiwa kwa kile alichodai ni mtindo uliyopo Bongo hasa upande wa wasanii.
"Siwezi kumueweka mpenzi wangu hadharani kwa sababu Wabongo ni wezi, wakimuona tu wananza kumsaka mwisho wa siku waniibie, hapana aisee!, lakini yupo na ninampenda sana" amesema.
"Kwanza ukiangalia ndani kumejaa, nje kumejaa, walioko nje wanataka kungia ndani na walioko ndani wanataka kutoka nje, basi tafrani kila mahali" amesema Recho.
Mwaka 2013 Recho alishinda tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) kama Msanii Bora wa Kike baada ya kuwabwaga Isha Mashauzi, Khadija Kopa, Lady Jaydee na Mwasiti.