Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, Manchester City wamepewa nafasi ya ya kumsajili mshambuliaji Cristiano Ronaldo kutokea Juventus.
Mkataba wa Ronaldo na Juventus mwisho mwa msimu ujao katika majira ya kiangazi hivyo wanahitaji kumuuza ili kupunguza gharama za mishahara kwani CR 7 anapokea paundi laki tano kwa wiki.
Wakala wa mchezaji huyo, Jorge Mendes anatafuta timu yenye uwezo wa kulipa kiasi cha paundi Milioni 25 ili kuinasa saini yake.
Imeripotiwa kuwa Manchester City ipo tayari kumlipa Ronaldo mshahara wa paundi Milioni 12.8 kwa mwaka
CR 7 aliifungia Manchester United mabao 118 katika michezo 292 katika miaka ya 2003 hadi 2009, amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka Juventus ingawa bado hajawasilisha maombi yake rasmi kwa uongozi wa mabingwa hao wa zamani wa Italia.
Imearifiwa kuwa wawakilishi wa Ronaldo wanapambana ili kuhakikisha Gabriel Jesus anakuwa sehemu ya mpango huo wa uhamisho lakini Manchester City haijakubali kumauchia mshambuliaji huo wa Brazil.
Pep Guardiola ameshakamilisha usajili wa Jack Grealish kwa paundi Milioni 100, na inawezekana akamsajili Ronaldo baada ya kumkosa Harry Kane ambaye jana alithibitisha ataendelea kuitumikia Tottenham Hotspurs.