KAMA ulikuwa hufahamu, basi tunaomba tukufahamishe japo tu sehemu ya mkataba wa mkali wa kusakata kabumbu duniani, Cristiano Ronaldo na klabu ya soka ya Manchester United aliyojiunga nayo wiki hii.
Mkataba wake ni wa muda wa miaka miwili ambapo atakuwa analipwa mshahara wa Euro 480,000 kwa wiki, kwa Shilingi za Kitanzania mchanguo wake ni kama ifuatavyo;
Atakuwa anapiga shilingi bilioni 1.44 kwa wiki, shilingi milioni 206 kwa siku, shilingi milioni 8.6 kwa saa, shilingi 143,000 kwa dakika na shilingi 2,380 kwa sekunde.