Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari na hadi sasa hakuna hata kimoja kilichowahi kulalamika.
Kiongozi mkuu huyo wa nchi ameeleza hayo wakati akihojiwa na mtangazaji Salim Kikeke wa BBC ambapo pamoja na mambo mengine aligusia masuala ya demokrasia na siasa.
“Wewe mwandishi wa habari toka umefika umesikia vyombo vya habari vimelalamika, hakuna chombo kinalalamika kuna uhuru wa kutosha na wanajieleza mpaka wanavuka mipaka saa nyingine, lakini kwa sababu kiongozi inabidi uvae ngozi ngumu muangalie,” amesema Samia alipoulizwa swali na Kikeke kuhusu uhuru wa kujieleza.
Rais Samia amesema kuwa bora umpe mtu nafasi ya kusema ili kiongozi ujue kinacholalamikiwa na kukifanyia kazi akisisitiza kuwa nchi ina uhuru wa kutosha na vyombo vya habari vyote vipo huru.
Akizungumzia demokrasia na siasa amesema kuna tofauti ya demokrasia ya kisiasa na fujo za siasa, “Demokrasia ya kisiasa ipo naomba nitofautishe demokrasia ya kisiasa na fujo ya kisiasa. Demokrasia ya kisisa ni nini ? Tuna vyama vya siasa, wana vyombo vyao wanajadili mambo yao kwa mfano baraza la vyama vya siasa huko wanajichangua wenyewe wanajadili mambo yao ya kisiasa, kuna kamati ya vyama vyenye wabunge bungeni nao wanao ya kwao, wanakaa wanazungumza wanaelewa.”
“Lakini kuna vyama vyenyewe vya siasa ambavyo vimeundwa na katiba zao na kufanya kazi kwao kunategemea na katiba zao. Kwa mfano chama changu cha mapinduzi (CCM), katiba yangu inaniambia labda katika mwaka nitakuwa na vikao viwili vya halmashauri kuu ya chama labda na vikao sita vya kamati kuu na vikao vingi katika ngazi za chini mikoa na wilaya na hivyo vikao vimeeleza wajumbe ni nani na kila kitu. Vinaendeshwa bila bugudha, bila kuomba ruhusa polisi kwa sababu katiba ishaeleza na imepita kote inajulikana na hivyo hivyo, vyama vingine vyote vina katiba zao, taratibu zao za mikutano na wajumbe wao ni kina nani, hivyo wako huru kufanya wakati wowote.”
Amesema jambo ambalo nalipendezi ni kutaka uhuru wa kufanya fujo za kisiasa, “labda tumemaliza uchaguzi Serikali imeundwa kinachotakiwa kuendelea ni kujenga nchi, uwe unachama gani uwe na chama gani wote mnakuja kwa pamoja mnajenga nchi yenu ndio kinachotakiwa kuwa.”
“Lakini inapotokea chama wao wanataka kuitisha maaandamano kila siku, maandamano yasiyo na mwisho..., maandamano sijui ya niniii..., labda leo mkutano, kesho mkutano fujo vurugu, kama ni uhuru wa kidemokrasia mbona Marekani au Ulaya hakuna wakimaliza uchaguzi ni kimya wanaendelea na shughuli zao za maendeleo.”
walijua mnyonge etii# hadi maji waite MMA
ReplyDelete