Tanzia: Daktari Massawe bingwa wa magonjwa ya watoto afariki dunia



Dar es Salaam. Daktari Bingwa mshauri wa magonjwa ya watoto wachanga Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Augustine Massawe amefariki dunia leo Ijumaa Agosti 13, 2021 wakati anapatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano kwa umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, “Amefariki saa mbili na nusu asubuhi leo.”

Dk Massawe ni daktari maarufu ambaye amekuwa akitibu watoto tangu mwanzoni mwa miaka ya 1980 na alipata umaarufu mkubwa katika jijini la Dar es Salaam kutokana na huduma ambayo alikuwa akiitoa.

Kutokana na kujituma kwake, licha ya kustaafu miaka 10 iliyopita Muhimbili ilimuomba aendelee kutoa huduma na hadi anafariki alikuwa bado akihudumia watoto hospitalini hapo na akiendelea kufundisha wanafunzi wa udaktari katika Chuo Kikuu kishiriki cha Afya na Sayansi Muhimbili (Muhas).

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Agosti 13, 2021 mtoto mkubwa wa marehemu DK Furaha Agosti amesema babayake alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upumuaji.

 
“Baba amefariki asubuhi ya leo alikuwa anaumwa na alilazwa Muhimbili kwa zaidi ya wiki na leo saa tatu asubuhi Mungu akamchukua,” amesema DK Furaha ambaye ni daktari wa magonjwa ya kina mama na uzazi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad