Trump amkosoa Biden jinsi alivyoshughulikia suala la Afghanistan katika mahojiano na kituo cha habari cha Fox News. Rais huyo wa zamani wa Marekani pia alikosoa kujiondoa kwa Joe Biden kutoka Afghanistan, na vile alivyoshughulikia suala la wanaovuka mpaka wa Mexico ambayo idadi yake hivi karibuni imepita ile iliyorekodiwa kwa kipindi cha miongo miwili.
“Angalia kile alichokifanya Biden katika mpaka wa kusini… [hali ilivyo nchini Afghanistan] ni kama mpaka wa kusini lakini imeshughulikiwa vibaya zaidi.
Hakuna mtu aliyeshughulikia suala la mpaka wa kusini vibaya zaidi kuliko yeye, Afghanistan vivyo hivyo“, amesema.
Bwana Trump pia alidai kwamba angeshughulikia uondoaji wa majeshi kwa njia tofauti.
“Nilipunguza [jeshi la Marekani nchini Afghanistan] kutoka karibu 20,000 hadi wanajeshi 2,500 – na [sasa wanaondoa] tena wanajeshi kabla hatujatoa raia wetu na wakalimani na watu wengine … waliotusaidia.
“Sasa basi, tulichokuwa tunatakiwa kufanya ni kuchukua wanajeshi wetu mwisho – watu walikuwa ni wawe wa [kwanza] kuondoka“, amesema.