Tunda Man : Kuna watu wapo nyuma ya Haji ambao hawapendi maendeleo ya Simba



Msanii wa bongo fleva Tunda man ameonyeshwa kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Haji Manara na kudai kuwa kuna watu wapo nyuma yake ambao hawapendi maendeleo ya Simba.
Kupitia ukurasa wake wa instagramu ameandika hivi;

Kifupi Sijapenda namna ambavyo rafiki yangu HAJI MANARA alivyoeleza kuhusu timu yangu pendwa hasa kwa maslahi ya baadae, kitendo cha kusema kuwa yeye ndio mtu pekee ambaye amesababisha SIMBA ikawa inajaza mashabiki kwa wingi ni kuwakosea heshima wote waliojitolea kuipambania SIMBA kwa moyo wao wote lakini pia kaonesha ubinafsi wa hali ya juu. Kwa mfano Mimi binafsi nimefanya mengi Kwa kutumia nafasi yangu na kipaji Changu kupitia Muziki kushawishi na kujenga hamasa ndani na nje ya SIMBA bila malipo yeyote na bado ni mwaminifu Kwa Simba Yangu!!

Ukisema SIMBA umeipigisha NDONDO ili tuu wachezaji wapate posho inaweza kuwa ni Jambo la kheri ndani Ila nje ya CLUB inajenga taswira hasi na kushusha hadhi ya CLUB kibiashara " brand". Pia unapo mshutumu Mwenyekiti "MO DEWJI " na CEO " @bvrbvra hadharani ambao kimsingi ni viongozi wa Taasisi kubwa ya SIMBA pasi kujali uhalali WA taarifa hizo ni kuidhalilisha Club na kuharibu mahusiano baina ya viongozi na future ya Simba Kwa Ujumla!!

Kuna wapenzi wengi wa Simba ambao wamekuwa wanaisaidia Club Kwa Hali na Mali bila kutaka hata Kutajwa majina Yao na wala hawajahi kufikiri kufanya Mkutano WA hadhara kusema madhaifu ya SIMBA kama alivyofanya my brother Haji!! Kwani naamini kulikuwa na njia nyingi na taratibu za kitaasisi ambazo MY BROTHER angezifuata na kuwasilisha hoja zake za msingi bila kuleta taharuki yeyote.

Imani yangu naamin kuwa kuna watu nyuma ya HAJI wasiopenda maendeleo na mafanikio ya Simba hivyo wametumia Hali hii Kutaka kuivuruga na kutenganisha mshikimano wetu Wana Msimbazi ili kufelisha malengo ya CLUB na kumvunja Moyo Kiongozi wetu @moodewji na kumtoa kwenye reli Kwa kusingizia sababu za ushindani Kibiashara na Umaarufu hata kama ni ushindani WA kibiashara ni upi na na Nani na kwa lipi Kwa maslahi ya Nani????

Pia my brother HAJI kumbuka kuna kesho na kuna tofauti kubwa Kati ya MTU binafsi na Taasisi hasa ukizingatia bado unahitaji fursa na kufanya kazi za Taasisi. Maneno ya Msemaji wa zamani ni ya kupuuzwa na kutupiliwa mbali kwani hayazingatii weledi wa utendaji kazi, yana nia ya kumkimbiza @moodewji ili asuse na kusababisha udhaifu kwenye timu na kuwapa nguvu zaidi washindani wetu!!" - TUNDAMAN.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad