Wizara ya Mambo ya nje nchini Ufaransa inasema, mpaka sasa hakuna kinachoashiria kuwa makabiliano ya risasi siku ya Jumatano kati ya maafisa wa polisi na mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki nje ya ubaozi wake jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na kusababisha vifo vya watu wanne, yalilenga ubalozi wake.
Tukio hili limesababisha hofu miongoni mwa wakaazi wa jiji la Dar es salaam, klingana na mwandishi wetu mwandishi wetu jijini Dar es Salaam Steven Mumbi.
Maafisa watatu wa polisi na askari 1 wa kampuni ya ulinzi ya SGA wakati wa shambulio hilo la risasi lililotokea katika barabara kunakopatikana balozi za kigeni jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji aliyekuwa alijihami kwa bunduki aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi mbele ya ubalozi wa Ufaransa. Kufikia sasa hajafahamika sababu za mtu huyo kufanya kitendo hicho.
Mamlaka ya Tanzania ilibaini Jumatano jioni kuwa ni mapema mno kuthibitisha kuwa shambulio hilo ni laugaidi, na kwamba walikuwa bado wanachunguza kilichosababisha mshambuliajihuyo anatekeleza kitendo hicho kiovu.