Timu ya taifa ya kikapu ya Marekani 'USA' imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Olympic baada ya asubuhi ya leo Agosti 5, 2021 kuifunga timu ya Australia kwa alama 97-78 na kutinga fainali hiyo kwa mara ya nne mfululizo.
Ushindi wa USA ulichagizwa na viwango bora vya nyota wake Kevin Durrant aliyeibuka kuwa nyota wa mchezo kwa kufikisha alama 23, rebaundi 9 na assist 2 huku Deniv Booker aliyefikisha alama 20, rebound 3 na assist 1 wakati Jrue Holiday alizoa alama 11, rebound 8 na assist 8.
Kwa upande wa Australia Mills Patty alitoa upinzani kwa Durrant lakini alama hazikutosha kuifanya timu yake iwazuie mabingwa hao watetezi wasitinge fainali hiyo kuwania medali ya dhahabu kwani Mills alipata alama 15, rebound 5 na Assist 8.
Exum Dante alikusanya alama 14, rebound 4 na assist 2 na Landale Jock akizoa alama 11, rebound 6 na assist 1 kwa upande wa Australia.
Sasa USA inasubiri bingwa wa mchezo wa saa 11:00 jioni ya leo wakati Ufaransa itakapocheza dhidi ya Slovenia.