Vifo vya vigogo saba katika wiki mbili vyashtua



Dar es Salaam. Tanzania imepoteza wafanyabiashara kadhaa katika siku za hivi karibuni ambao wamejizolea maarufu katika sekta mbalimbali.

Kifo cha Mwenyekiti wa Kampuni za Asas Group, Alhaj Faraj Ahmed Abri kilichotokea siku tatu zilizopita jijini Dar es Salaam kimeongeza pigo kwa jumuiya ya wafanyabiashara baada ya kufikisha idadi ya watu maarufu sita waliofariki dunia katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Mwili wa Mwenyekiti wa kampuni za Asas Group Of Companies, Alhaj Faraj Ahmed Abri umezikwa jana katika makaburi ya Kisutu na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, akiwemo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Wengine waliofariki katika kipindi hiki ni mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite, Mathias Manga aliyewahi kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), akiwa nchini Afrika Kusini.


 
Pamoja na umiliki wa mgodi wa Tanzanite wa Manga Gems uliopo kitalu D, marehemu Manga aliyefariki dunia juzi pia alikuwa anaendesha Hoteli za Gold Crest zilizopo jijini Arusha na Mwanza na alikuwa anamiliki majumba kadhaa ya kifahari jijini Arusha.

Mwingine ni mfanyabiashara maarufu Tanil Kumar Somaiya aliyefariki dunia siku nne zilizopita jijini Dar es Salaam na aliwekeza katika mawasiliano kupitia Kampuni ya Shivacom na Ulinzi (Ultimate Security).

Wengine ni aliyekuwa mmiliki wa hoteli ya Peacock, Joseph Mfugale aliyefriki dunia Julai 31, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Mfugale ni miongoni mwa wamiliki wa hoteli wazawa aliyepata mafanikio katika biashara hiyo, akifungua hoteli Dar es Salaam na nyingine mkoani Iringa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad