Kituo cha Televisheni cha Kimataifa cha CNN cha nchini Marekani kimewafukuza kazi Watumishi wake watatu kwa kukiuka sera ya kampuni hiyo kwa kuingia kazini bila ya kuwa wamechanja chanjo dhidi ya Covid-19.
Mapema jana Alhamisi, Mkuu wa CNN, Jeff Zucker aliwakumbusha kwa maandishi Wafanyakazi wa kituo hicho kwamba chanjo ni lazima kama watapaswa kufika kazini, hata hivyo uongozi wa kituo hicho haujatoa taarifa zaidi kuwahusu waliofukuzwa, au hata vituo vyao vya kazi.
Kutokana na hali tete ya maambukizi ya virusi vya Corona kituo hicho cha Kimataifa kimesitisha mpango wake wa kuwarejesha Wafanyakazi wake kwa kiwango kikubwa, kama ilivyokuwa imepangwa awali September 7, kwa hivyo zoezi hilo linatarajiwa kufanyika katikati ya October.
Kwa zingatio la sababu kama hiyo vyombo vingine vya habari vimefuata mkondo kama huo.