Waliyochanjwa ruksa Umrah, Saudi Arabia




Saudi Arabia itaanza kuwapokea wageni waliopata chanjo ya Covid-19 katika mji mtukufu wa Kiislamu wa Makka ikiwa kama sehemu ya ibada ya umrah. Ni takriban miezi 18 tangu kuifunga mipaka yake baada ya kuzuka janga la virusi vya corona.



Shirika la habari la Saudia limesema Wizara ya Hijja na Umrah imetangaza kuanzia kesho Jumatatu watapokea maombi ya raia na wakazi wake wanaotaka kushiriki ibada ya Umrah.

Lakini pia baadae watapokea maombi kutoka mataifa mbalimbali ya nje. Ruhusa hiyo hata hivyo imetolewa kwa masharti kwamba mahujaji wote wa kigeni lazima wawe wamepigwa chanjo inayotambuliwa na Saudi Arabia na wakubali kukaa karantini.

Ibada ya Umrah ambayo kwa kawaida inafanyika katika kipindi chochote cha mwaka, ilifunguliwa tena Oktoba kwa mahujaji wa ndani, baada ya kufungwa kabisa kutokana na mripuko wa janga la virusi vya corona.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad