Watu wanaoaminika kuwa wanamgambo wa kijihadi wameuwa watu 47 katika shambulio dhidi ya msafara wa jeshi nchini Burkina Faso, baadhi ya wahanga wakiwa raia. Wizara ya habari ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi imethibitisha tukio hilo, na kusema limetokea karibu ya mji wa Arbinda.
Tangazo la wizara hiyo limesema washambuliaji kadhaa pia walipoteza maisha katika majibizano ya risasi.
Kwa miaka kadhaa sasa nchi tatu za ukanda wa Sahel, Burkina Faso, Niger na Mali zimekuwa zikisumbuliwa na mashambulizi ya wanamgambo wa kijihadi, walio na mafungamano na mitandao ya kimataifa ya kigaidi.
OPEN IN BROWSER