Watu watatu wauawa Bagamoyo





  Watu watatu wamefariki dunia katika matukio tofauti yakiwemo ya ubakaji, tuhuma za ushirikina pamoja na mgogoro wa ardhi katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema hayo leo Agosti 9, 2021 mjini Kibaha wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu msako wa kudhibiti matukio ya uhalifu walioufanya kwa siku saba kwenye mkoa huo.


Akieleza matukio hayo amesema la ubakaji limetokea Agosti 8 saa tisa alasiri Kijiji cha Tobora Msata ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 26 alibakwa kisha kuuawa na mwili wake kutupwa vichakani.


Nyigesa amesema wamemkamata mtuhumiwa mmoja na anaendelea kuhojiwa ambapo mara baada ya upelelezi majina yao yatatajwa na hatua zaidi za kufikishwa mahakamani zitafanyika.


"Kwa sasa hatuwezi kutaja majina ya watuhumiwa, kwa sababu bado tunaendelea na upelezi,"amesema Nyigesa.


Katika tukio la pili bibi mmoja  (70) jina pia linahifadhiwa mkazi wa kijiji cha Kitonga Bagamoyo ameuawa na kisha kukatwa katwa na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili chake kwa kadai ya kuhusishwa na ushirikina.


Nyigesa amebainisha tukio hilo limetokea saa 12 jioni juzi ambapo baada ya kufanyiwa ukatili huo mwili wake ulitupwa vichakani, hata hivyo tayari mtuhumiwa mmoja anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad