Zambia: Hichilema achukua uongozi wa mapema dhidi ya Rais Lungu





Matokeo ya kwanza yaliyotolewa leo Jumamosi na tume ya uchaguzi ya Zambia yanaonyesha kuwa kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema, amechukua uongozi wa mapema dhidi ya Rais aliyeko madarakani Edgar Lungu.
 
Hichilema amepata kura 171,604 dhidi ya kura 110,178 alizozipata Lungu katika matokeo ya maeneo bunge 15 kati ya 156 ya taifa hilo la kusini mwa Afrika.
 
Matokeo katika maeneo bunge hayo ambayo yanatajwa kuwa ni ngome za Lungu, yanaashiria kuwa Hichilema amepata uungwaji mkono mkubwa katika ngome za mpinzani wake tofauti na uchaguzi wa mwaka 2016 uliogubikwa na madai wa wizi wa kura.Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Patrick Nshindano, amewaambia waandishi habari mjini Lusaka kuwa jumla ya kura 296,210 zilipigwa katika maeneo bunge hayo.
 
Matokeo ya kwanza yaliyotarajiwa kutolea jana Ijumaa yalichelewa baada ya zoezi la kuhesabu kura kuendelea hadi usiku kutokana na idadi kubwa ya wapiga kura, na pia kwa sababu baadhi ya vyama vya kisiasa vilipinga matokeo yaliyotolewa na tume hiyo katika eneo bunge moja.
 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad