Zitto: Chanjo ya corona ni salama, wananchi kachanjeni



Dar es Salaam. Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amepongeza Serikali kuruhusu chanjo, ili Watanzania wapate kinga dhidi ya ugonjwa wa Covid 19, huku akiwahakikishia wanachama wa chama hicho kuwa zipo salama.

Zitto ameeleza hayo  leo Jumapili Agosti 8,2021 katika hotuba yake kwa Taifa wakati wa ufunguzi wa kikao cha kamati kuu kinachoendelea Mjini Unguja.

 “Napenda kuwahakikishia nimejiridhisha chanjo zilizoruhusiwa kuingia nchini ni salama na mimi nimeshachanjwa, niko salama. Nipende kuwaasa kuwa kuchanjwa ni suala la hiari, lakini tunapoangalia usalama wa wapendwa wetu, jamii yetu na Watanzania wenzetu, hatuna budi kufanya uamuzi sahihi,” amesema Zitto

Licha ya kupongeza uamuzi huo, kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya kwenye uhamasishaji wa watu kujitokeza kupata chanjo.

 Zitto amesema lazima kuwepo na mkakati maalumu wa uhamasishaji wa kupata chanjo utakaongozwa  watu wanaoaminika kwenye jamii, na sio wale wale waliosema  Tanzania imeishinda  vita dhidi ya ugonjwa huo kwa kutumia dawa za asili.

“Tuendelee kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuepuka mikusanyiko, kuvaa barakoa na kunawa kwa maji tiririka na sabuni kila wakati pamoja na kutumia vitakasa mikono.Serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar zichukue  hatua madhubuti  za kuongeza elimu kwa wananchi  ambao kwa nyakati tofauti waliambiwa hakuna corona,” amesema Zitto.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad