Abiria wakosa usafiri baada ya nahodha wa kivuko kuugua




Abiria wanafanya Safari ya kwenda mitaa ya mitumbikwera akigombea kiboti baada ya boti Mv kitunda kushindwa kusafirisha abiria kutokana na nahodha kuumwa.
Lindi. Baadhi ya wakazi wa Kata ya kitumbikwera mkoani hapa wamekwama kusafiri tangu asubuhi baada ya kivuko ya MV Kitunda kushindwa kufanya safari kwa sababu ya kukosa nahodha.

Wakizungumza na Mwananchi leo Septemba 13, 2021 mjini Lindi, baadhi ya wakazi wamesema wameshindwa kurudi kwao baada nahodha wa kivuko kuja eneo la kazi na kuondoka kwa madai anaumwa.

“Tumekuja asubuhi na mapema na mitumbwi baada ya kuambiwa kuwa kivuko hakifanyi kazi kwa kuwa nahodha anaumwa, imetushangaza kwa kweli,” amesema Mohamed Karim.  

Ameongeza: “Taasisi kubwa kama hii inawezaje kuwa na nahodha mmoja tu? Maana Mimi nina biashara ya nyanya hapa sasa tangu asubuhi niko hapo nashindwa kusafiri kwa mitumbwi kwa kuwa mzigo wangu mkubwa.”


 
Naye Asia Juma mkazi wa mtaa wa Sinde amesema wanachangamoto ya usafiri tangu asubuhi iliyosababisha abiria kutoka Lindi mjini kuvuka upande wa Kitunda kushindwa kusafiri kwa wakati hali ambayo imesimamisha shughuli zao.

“Tunaiomba Serikali kuangalia kivuko hiki mara kwa mara kwani kuna wanawake wajawazito na wagonjwa wanaoishi Kitunda wanaohitaji kwenda hospitali ya Mkoa ya Sokoine,” ameema Asia.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Mkoa wa Lindi, Rocky Sabigoro amekiri kusimama kwa kivuko hicho na kueleza kutokana na upungufu wa nahodha baada anayendesha kuugua.


"Ni kweli kivuko kimesimama kusafisha tangu asubuhi baada ya kukosa nahodha"kwani nahodha aliyekuwepo anapata dharura ya kuumwa.

“Tumeamua kutumia kivuko kidogo cha dharura ili kupunguza kero hiyo wakati, tukiomba msaada wa kuletewa nahodha wa mwingine ili wawe wawili.alisema Meneja huyoo,” amesema Sabigoro.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad